Rais Uhuru Kenyatta yuko mjini New York, Marekani kwa ziara rasmi ya siku mbili.

Rais ameratibiwa kuongoza mkutano wa ngazi za juu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuangazia amani.

Mwakilishi wa Kenya katika Umoja wa Mataifa UN Martin Kimani anasema ajenda ya baraza hilo la usalama ni kujadili mikakati ya kuleta amani na usalama katika mataifa ya upembe wa Afrika na eneo la Sahel.  

Rais Kenyatta vile vile ameratibiwa kufanya mazungumzo na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress na kushuhudia kutia saini kwa makubaliano ya kibiashara na kampuni za Marekani.