Tume ya uchaguzi na mipaka nchini (IEBC) imemteua Juliana Cherera kuwa naibu mwenyekiti mpya.

Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati amesema kuwa Cherera ameteuliwa kwa kauli moja katika kikao kilichoandaliwa leo.

Chebukati amewahakikishia wadau wote kwamba tume hiyo iko mbioni kufanikisha maandalizi ya uchaguzi huru na haki.

Cherera ni miongoni mwa makamishna wanne walioteuliwa na rais Uhuru Kenyatta ambaye aliahidi kujali maslahi ya wakenya kwa kuandaa chaguzi zenye amani.