Maafia sita wa Polisi wameshtakiwa kwa mauji ya ndugu wawili wa Kianjokoma wameshtaka kwa mauji.
Hata hivyo wamekanusha mashtaka mbele ya jaji Daniel Ogembo.
Washukiwa hao watazuiliwa katika magereza ya Industrial Area na Lang’ata hadi Septemba 22 wakati mahakama itasikilzia ombi lao la kuachiliwa kwa dhamana.
Kupitia kwa wakili wao Dunstan Omar aliyejiondoa kabla ya kurudi tena washukiwa waliimabia mahakama kwamba taratibu zinazofaa hazikufuatwa kabla yao kufikishwa mahakamani.
Omar amepinga madai kuwa wanalenga kuchelewesha kesi hiyo na kuonya kuwa iwapo itaendelea mbele, itatumika visivyo kuwahukumu polisi wengine iwapo washukiwa watafariki mikononi mwao.
Sita hao Benson Mputhia, Consolata Kariuki, Nicholas Cheruyoit, Martin Wanyama, Lilian Chemuna na James Mwaniki wanatazamiwa kujibu mashtka ya kumuua Benson na nduguye Emmanuel Ndwiga.