Mahakama imeagiza Polisi SITA waliokamatwa kuhusiana na mauaji ya ndugu wawili wa Kianjokoma kaunti ya Embu wakule kiapo.

Jaji Daniel Ogembo amefutilia mbali ombi la Polisi hao kutaka wasikule kiapo hadi kesi waliyowasilisha mahakamani kupinga kushtakiwa kwao isikilizwe.

Washukiwa hao wanatazamiwa kula kiapo Alhamisi wiki hii hatua itakayotoa nafasi kwa serikali kuwapata mawakili baada ya mawakili wao Danston Omar na Cliff Ombeta kujiondoa.

Sita hao ni; Benson Mputhia, Consolata Kariuki, Nicholas Cheruyoit, Martin Wanyama, Lilian Chemuna na James Mwaniki.