Hakuna yeyote anayeruhusiwa kutoa chanjo ya corona mbali na wizara ya afya ameonya waziri Mutahi Kagwe.

Huku akitoa wito kwa Wakenya kuendelea kujitokeza kupata chanjo, Waziri Kagwe anasema ni wizara ya afya pekee ndiyo ina jukumu la kutoa chanjo hiyo na maafisa walioidhinishwa.

Waziri wa afya amewakanya wanasiasa dhidi ya kuingiza siasa katika zoezi hilo la akisema hatua hiyo inahatarisha maisha ya Wakenya.

Waziri Kagwe pia amewataka Wakenya wasikubali kulipa pesa zozote ili kupata chanjo na kuagiza kufungwa kwa vituo vya afya vinavyoitisha pesa ili kutoa chanjo.

Wakati uo huo

Kenya imeripoti maambukizi mapya 346 ya ugonjwa wa corona baada ya kupima sampuli 3,553.

Hii inafikisha idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini kuwa 235,298, kiwango cha mambukizi kikiwa katika asilimia 9.7%.

Waziri ya afya Mutahi Kagwe anasema watu wengine 1,404 wamepona na kufikisha idadi hiyo 222,357 huku kwa mara nyingine akiwataka wanasiasa kukomesha mikutano ya hadhara.

Idadi ya maafa imefikia 4,720 baada ya kufariki kwa wagonjwa 10 zaidi.