Wabunge wameitwa kwenye kikao maalum Jumatano hii kuidhinisha majina ya makamishna wateule wa tume ya uchaguzi (IEBC).

Karani wa bunge la kitaifa Michael Sialai amesema bunge litakabidhiwa ripoti ya kamati ya haki na maswala ya kisheria iliyowasaili wanne hao wakati wa kikao hicho.

Wabunge vile vile wanatazamiwa kupokea ripoti kutoka kwa kamati ya elimu kuwahusu wanachama wateuliwe wa tume ya huduma za walimu (TSC).

Rais Uhuru Kenyatta aliwateua Juliana Cherera, Francis Wanderi, Irene Masit na Justus Nyang’aya kuwa makamishna wapya wa IEBC.

Walioteuliwa kuwa makamishna wa TSC ni; Dr Nicodemus Anyang, Christine Kahindi, Sharon Kisire, Anneta Wafukho na Salesa Abudo.