Naibu rais William Ruto amenyanganywa walinzi wake.

Maafisa wa GSU waliokuwa wanalinda makaazi ya Ruto Karen, Nairobi na nyumbani kwake Sugoi wameondolewa na nafasi yao kutwaliwa na wenzao wa AP.

Idara ya Polisi haijatoa taarifa kamili kuhusu ni kwa nini hatua hiyo imechukuliwa.

Maafisa hao wanaondolewa wakati ambapo tofauti baina ya rais Uhuru Kenyatta na naibu wake zimeonekana hadharani hali ambayo imemfanya rais kumtaka naibu wake kujiuzulu kama amechoka.