Maafisa sita wa Polisi wanaohusishwa na mauaji ya ndugu wawili wa Kianjokoma kaunti ya Embu wamewasilisha kesi mahakamani kuzuia kushtakiwa kwao.

Kupitia kwa wakili wao Danstan Omar, Polisi hao wameutaka upande wa mashtaka usiwafungulie mashtaka ya mauji na kutaka kuachiliwa kwa dhamana.

Sita hao Benson Mputhia, Consolata Kariuki, Nicholas Cheruyoit, Martin Wanyama, Lilian Chemuna na James Mwaniki aidha wanataka uchunguzi zaidi kufanyika na miili ya wawili hao Benson na Emmanuel Ndwiga kufufuliwa ili upasuaji ufanyike mbele yao.