Kenya imedhibitisha maambukizi mapya 1,258 ya ugonjwa wa corona baada ya kupima sampuli 9,868.

Hii inafikisha 232,052 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini kiwango cha maambukizi kikiwa 12.8%.

Watu 753 zaidi wamepona na kufikisha idadi hiyo kuwa 216,127 huku wagonjwa 36 zaidi wakifariki na kufikisha idadi hiyo kuwa 4,600.

Wagonjwa waliolazwa ni 1,941 katika hospitali mbalimbali, wanaoshughulikiwa nyumbani wakiwa 8,126.

Yakijiri hayo

Viongozi wa kidini wametakiwa kuwa katika mstari wa mbele kuwahimiza Wakenya kujtokeza kupata chanjo ya ugonjwa wa corona.

Wito huu umetolewa na naibu rais William Ruto ambaye amesema viongozi hao wana nafasi nzuri kutoa elimu kwa umma ili kufanikisha vita dhidi ya ugonjwa huo.

Ruto amesema haya alipokutana na viongozi wa kanisa la African Independent Pentecostal Church of Africa (AIPCA) kutoka Murung’a katika afisi zake za Karen, Nairobi.