Kongamano la saba la Ugatuzi lililokuwa liandaliwe wiki ijayo Agosti 23-26 katika kaunti ya Makueni limehairishwa kwa sababu ya corona.

Akisema kuwa tarehe mpya itatangazwa baadaye, mwenyekiti wa baraza la magavana Martin Wambora amesema wamelazimika kuchukua hatua hiyo kwa sababu ya kuongezeka kwa msambao wa ugonjwa wa covid-19.

Haya yanajiri siku moja baada ya rais Uhuru Kenyatta kupiga marufuku mikutano ya aina yoyote katika juhudi za kudhibiti maambukizi mapya huku kaunti ya Makueni ikiwa miongoni kwa maeneo yanayoripoti idadi kubwa ya maambukizi mapya ya ugonjwa huo.