Kenya imeripoti maambukizi mapya 1,506 ya ugonjwa wa corona baada ya kupima sampuli 9,840 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Hii inafikisha 224,400 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini kiwango cha maambukizi kikiwa asilimia 15.3%.

Watu 1,538 wamepona na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 207,450 huku idadi ya maafa ikiongezeka na kufikia 4,378 baada ya kufariki kwa wagonjwa 24 zaidi.

Wagonjwa 2,054 wamelazwa katika hospitali mbalimbali wengine 8,408 wakishughulikiwa nyumbani.