Rais wa Zambia wa Edgar Lungu amekubali kushindwa kwenye uchaguzi uliokamilika hivi punde.

Rais Lungu kwenye hotuba kwa taifa amesema jukumu lake litakuwa ni kufanikisha mpito wa mamlaka kwa njia ya amani kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.

INSERT: LUNGU ON KUSHINDWA

‘’Asanteni Wazambia wenzangu kwa kunipa fursa ya kuwa rais wenu. Nitafuata katiba katika kuhakikisha mpito wa mamlaka kwa njia ya amani. “Nachukua furasa hii kumpongeza ndugu yangu Hakainde Hichilema kwa kuchaguliwa kuwa rais wa saba wa Zambia”.

Lungu hapo awali alikuwa amedokeza kwamba atapinga matokeo ya uchaguzi baada ya kushutumu upinzani kwa ulaghai.

Rais mteule Hakainde Hichilema amekaribisha ushindi huo akisema umefanikishwa kwa sababu ya juhudi za pamoja za wanazambia.

INSERT: HICHILEMA ON USHINDI

‘’Wapiga kura wameamua atakayewaongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijyao, ushindi huu sio wangu, ushindi huu ni wa raia wa Zambia haswaa vijana, nasisitiza kwamba ushindi huu ni wa vijana wa taifa hili’’.

Hichilema amethibitishwa mshindi katika uchaguzi wa urais, kwa kupata kura 2,810,777 dhidi ya Lungu aliyepata kura 1,814,201.