Kinara wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi amezindua ajenda yake ya kiuchumi anapojiandaa kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu wa 2022.

Mudavadi anasema taifa halihitaji mifumo ya kiuchumi ila kushiriki mazungumzo na wafanyibiashara kufahamu changamoto wanazopitia kwa makusudi ya kuleta sera zitakazowawezesha kunawiri.

Na huku joto la kisiasa likionekana kushika kasi, Mudavadi anawasihi Wakenya kuwachagua viongozi kwa kuzingatia suluhu wanazotoa kwa matatizo yanayowakumba.