Mtoto wa siku saba ni miongoni mwa watu 745 waliokutwa na ugonjwa wa corona baada ya kupima sampuli 6,209.

Idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini imeongezeka na kufikia 212,573 huku kiwango cha maambukizi kikiwa 12%.

Katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita, watu 161 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 197, 468.

Maafa yanazidi kupindukia huku wagonjwa 30 wakifariki na kufikisha idadi hiyo kuwa 4,173.

Wagonjwa waliolazwa katika chumba cha watu mahututi ICU 135, 61 wakisaidiwa na machine kupumua.