Mkenya Faith Kipyegon ametetea DHAHABU yake kwenye mashindano ya Olimpiki ya mita 1,500 kwa akina dada mjini Tokyo, Japan.

Kipyegon ambaye ameweka rekodi mpya amewaonyesha kivumbi Laura Muir na Sifan Hassan wa Uholanzi na kuishindia Kenya nishani ya pili ya DHAHABU.

Mwanariadha huyo alishinda dhahabu yake ya kwanza katika mashindano ya Rio mwaka 2016.

Kwenye fainali za mbio za mita 5,000 kwa wanaume, Mkenya Nicholas Kimeli alimaliza wa nne na hivyo dhahabu kumuendea Joshua Cheptegei wa Uganda.