Viongozi wanaendelea kurushiana cheche za maneno kufuatia kukatizwa kwa ziara ya naibu nchini Uganda Jumatatu.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kutokea kwa tuki hilo, Ruto amesema hatua ya kunyimwa nafasi na serikali kufanya ziara ya kibinfasi katika taifa hilo jirani ni njama ya kumdumdhalilisha.

Akihojiwa na kituo cha Inooro, Dr Ruto ambaye amekiri kutengwa na serikali amesema masaibu yake yalichangiwa na baadhi ya watu serikalini ambao wako kwenye mashindano ya ubabe.

Ruto ambaye safari yake iliishia katika uwanja wa ndege wa Wilson anawashtumu maafisa hao kwa kutaka kumkosanisha na Rais Uhuru Kenyatta baada ya kudaiwa kuwa aliambiwa atafute idhini kutoka kwa afisi yake.

Wakati u o huo

Chama cha ODM sasa kinamtuhumu niabu rais William Ruto kwa kulenga kutumia nguvu kunyakua uongozi.

Baadhi ya wabunge wa chama hicho wakiongozwa na Junet Mohammed wa Suna Mashariki wanadai kwamba safari ya Ruto kwenda Uganda ilikatizwa kwa sababu alilenga kujifunza mbinu za mkato kuingia mamlakani.

Wakati uo huo

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi ambaye ni mwendani wa Ruto ameitaka serikali kukoma kumuaibisha naibu rais William Ruto.

Sudi akiwahutubia wanahabari nyumbani kwa Uasin Gishu ametetea ziara binafsi ya Uganda huku akipuuzilia mbali madai kwamba walikuwa waandamane na mfanyibiashara anayehusishwa na ugaidi.