Maafisa wa polisi mjini Kiambu wanachunguza kisa ambapo wanandoa walipatikana wamefariki ndani ya nyumba yao.

Miili ya mfanyibiashara Jonathan Gachunga na mkewe Philomena Njeri wenye umri wa miaka 42 na 30 mtawalia ilipatikana ndani ya chumba cha kulala na majertaha ya risasi.

Polisi wanaamini kuwa Gachunga alimpiga risasi tatu ya kichwa mkewe kufuatia ugomvi wa kinyumani kabla ya kujipiga risasi ya kichwa pia.

Marafiki wa wawili hao wanasema mara ya mwisho waliwaona wanandoa hao walikuwa na furaha hawakuhisi dalili zozote za mgogoro baina yao.

Mkuu wa polisi Kiambu Ali Nuno amesema walipata bastola aina ya Glock ambayo huenda mshukiwa alitumia kutekeleza mauaji hayo.