Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Holy Trinity iliyoko Saboti kaunti ya Trans Nzoia amelazimika kupeleka jogoo shuleni baada ya kukosa karo inayogharimu Sh34,000.

Mathews Simiyu amesema hakuwa na lingine la kufanya kwa sababu alifukuzwa shuleni kuleta karo anayosema amekuwa akihangaika nayo kwa mwa mmoja sasa.

Licha ya kuwa mwerevu kwenye masomo yake, Simiyu hana sare za shule wala vitabu vya kusoma mwalimu mkuu wa shule hiyo akisema imekuwa vigumu kumsaidia mwanafunzi huyo.

Wakati uo

Wanafunzi wa kidato cha kwanza wameanza kuripoti shuleni Jumatatu huku shule zikiimarisha mikakati ya kuzuia maambukizi ya corona.

Kwa mfano katika shule ya Kenya High ambayo inatazamiwa kuwapokea wanafunzi zaidi ya mia tano, mwalimu mkuu Florence Mulatya amesema wameweka mikakati iliyopendekezwa na wizara ya Afya ikiwemo kuvaa barakoa, kutumia vieuzi na kudumisha usafi.