Polisi wamewaua kwa kuwapiga risasi washukiwa wawili wa utekaji nyara katika eneo la Kilimani, Nairobi.

Washukiwa hao waliojihami kwa bastola walikuwa wamemteka nyara dereva mmoja na mteja wake ambapo walikuwa wamewaibia simu zao na kuchukua usukani wa gari lao.

Polisi waliwazuia kwenye barabara ya Chania Avenue na kuwaagiza kujisalimisha.

Hata hivyo walikaidi agizo hilo na kuanza kuwafyatulia Polisi risasi wakijaribu kutoroka kwa miguu.

Makabiliano hayo yaliishia katika kuuawa kwa majambazi hao na kupatikana kwa simu nne na risasi ambazo hazikuwa zimetumika.

Miili yao imepelekwa katika hifadhi ya City.