Serikali imetangaza kukaza kamba katika masharti ya kuzuia msambao wa virusi vya corona kufuatia kuongezeka kwa idadi ya visa hivyo.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe ametangaza kwamba kafyuu ya kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri itasalia kuwepo katika kaunti mbalimbali ikiwemo kaunti za Nyanza huku mikutano ya kisiasa ikisalia kupuigwa marufuku.

Maabadi yataendelea na ibada ila kwa kuzingatia masharti ya usalama yaliyotolewa na baraza linaloongozwa na askofu Anthony muheria ikiwemo waumini kutokaribiana.

Na huku wanasiasa wakionekana kuwa katika mstari wa mbele kukaidi maagizo ya usalama na kuendelea na mikutano yao, Inspekta wa Polisi Hillary Mutyambai ameonya kwamba maafisa wa usalama hawatazembea katika kutekeleza maagizo ya usalama.

Waziri Kagwe ameagiza matanga kuhudhuriwa na watu hamsini pekee huku shirika la KEMRI likitakiwa kupeana vifaa vya kujikinga PPEs kwa serikali za kaunti pasipo kuzingatia madeni wanayodaiwa.