Madaktari wa Kenya hawana kazi watakuwa na nafasi kutafuta kazi nchini Uingereza kufuatia makubaliano mapya baina ya mataifa haya mawili.

Makubaliano hayo yametiwa saini baina ya waziri wa afya wa Uingereza Sajid Javid na mwenzake wa Leba wa Kenya Simon Chelugui kufuatia ombi la rais Uhuru Kenyatta.

Makubaliano hayo yatawapa fursa zaidi ya wahudumu afya 5,000 ambao hawana ajira kujaribu bahati yao nchini Uingereza.

Rais Kenyatta pia ameshuhudia kutiwa saini kwa makubaliano yatakayowezesha ushirikiano wa asasi mbalimbali za afya kati ya Kenya na Uingereza.