Msako umeanzishwa kutafuta genge la majambazi wanaodaiwa kutekeleza wizi kwenye benki ya Equity tawi la Matuu kaunti ya Machakos.

Walioshuhudia wanasema genge hilo la wezi watatu walivamia polisi wawili waliokuwa wanachunga benki hiyo na kuwanyanganya bunduki zao kabla ya kujitoma ndani na kulazimisha kila mtu kulala chini.

Wezi hao kisha waliiba pesa na kutoroka na bunduki za askari hao ambao wamebakia kuhadithia kilichojiri.

Maafisa wenzao walifika kwa wakati na makabiliano makali ya risasi yakazuka kabla ya wakora hao kutoroka.