Huku shule zikifunguliwa kwa muhula wa kwanza, walimu wakuu wameonywa dhidi ya kuwafukuza wanafunzi kwa kukosa karo.

Hussein Khalid, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Haki Afrika anasema wazazi wengi wanahangaika kwa sababu hakukuwa na muda wa kutosha kutafuta karo.

Khalid vile vile ameitaka serikali kuhakikisha kwamba wanafunzi wanapewa vitabu vya kusoma badala ya kuwaachia wazazi mzigo huo wakati ambapo hata ni vigumu kupata pesa za kununua chakula.

Tukisalia na hayo ya elimu

Walimu wapatao 73 wamefariki kutokana na virusi vya corona hadi kufikia sasa kwa mujibu wa takwimu kutoka tume ya huduma za walimu TSC.

Mwenyekiti wa TSC Dr Jamleck Muturi na afisa mkuu mtendaji Nancy Macharia wametoa wito kwa walimu kuhakikisha kuwa wanapokea chanjo dhidi ya corona ili kujiweka salama wasipatwe na virusi hivyo.