Wanahabari wamezuiwa kuchapisha taarifa, kutangaza, kujadili au kuhudhuria vikao vya kesi ambapo spika wa bunge la seneti Ken Lusaka ameshtakiwa kwa madai ya kutelekeza majukumu yake ya ulezi.

Hakimu Mkaazi wa Mahakama ya Milimani F Terer ametoa uamuzi huo kufuatia ombi la mwanamke aliyemshtaki spika huyo.

Mwanamke huyo kupitia kwa wakili wake Dunstan Omar alifaulu kuishawishi mahakama kuwazuia wanahabari kwenye kesi hiyo.

Kesi hiyo iliratibiwa kutajwa Jumatano wiki hii baada ya Lusaka kuomba kusuluhisha kesi hiyo nje ya mahakama.

Mwanamke huyo anataka Lusaka kumlipa shilingi million 25 ili kumlea mtoto huyo ambaye tayari baada ya spika huyo kukiri kuwa mimba aliyoibeba mwanamke huyo ni yake.