Chama cha United Democratic Alliance (UDA) kimetishia kuwasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa chama cha Jubilee kwenye uchaguzi mdogo wa wadi ya Muguga.

Ajenti mkuu wa chama hicho kwenye uchaguzi huo James Gacheru amewaambia waandishi wa habari kwamba wataiomba mahakama iagize kuhesabiwa upya kwa kura zilizokataliwa wakisema nyingi zilikuwa za muwaniaji wao.

Muwaniaji wa UDA Peter Thumbi aliyepata kura 4,062 alishindwa na Joseph Githinji wa Jubilee kwa kura 27 aliyetangazwa mshindi baada ya kupata kura 4,089.