Maambukizi mapya 618 ya ugonjwa wa corona yamedhibitishwa nchini baada ya kupima sampuli 5,507 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.  

Wizara ya afya imearifu kuwa hii inafikisha 193,807 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini huku kiwango cha maambukizi kikiwa 11.2%.

Wagonjwa wengine 290 wamepona na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 183,211 huku wengine 17 wakifariki na kufikisha idadi hiyo kuwa 3,800.

Idadi ya waliolazwa katika hospitali mbalimbali ni 1,222 huku wengine 4,339 wakishughulikiwa nyumbani.