Kesi ya mauaji dhidi ya wakili Willie Kimani imerejelewa Ijumaa huku afisa wa Polisi Nicholas Ole Sena akitoa ushahidi wake.

Akifika mbele ya jaji Jessie Lessit, Sena amesema kwamba mshukiwa wa tatu Sylviah Wanjiku alikuwa kwenye zamu katika kituo cha Syokimau walipozuiliwa Kimani pamoja na wenzake wawili.

Hata hivyo afisa huyo amekuwa na wakati mgumu kudhibitisha kwamba mshukiwa wa nne kwenye kesi hiyo alikuwa na nia ya kumuua Kimani pamoja na wenzake Josphat Mwenda na Joseph Muiruri.

Vikao hivyo vimehairishwa hadi Alhamisi ijayo Julai 22.