Maambukizi ya ugonjwa wa corona nchini yamepanda tena huku taifa likiandikisha visa vipya 761 kati ya sampuli 5,794 zilizopimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema hii inafikisha idadi ya visa hivyo kuwa 189,703 huku kiwango cha maambukizi nchini kikiwa katika asilimia 13.1%.
Waliopona katika muda huo ni 71 na kufikisha idadi hiyo kuwa 180,624 huku wagonjwa 9 zaidi wakifariki na kufikisha idadi hiyo kuwa 3,732.
Wagonjwa 1,067 wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini huku wengine 4,359 wakishughulikiwa nyumbani.