Ushahidi uliowasilishwa mahakamani umeonesha namna Sharon Otieno,26, mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo alivyopitia mateso kabla ya kukata roho.

Mpasuaji aliyekagua mwili wa marehemu ameimbia mahakama namna Sharon na mwanawe wa wiki 28 walivyoteswa na wauaji waliotekeleza unyama huo Novemba 3, 2018.

Novemba mwaka 2017 ndio wakati mahakama imeambiwa kuwa Gavana wa Migori Okoth Obado walikutana na Sharon Otieno, mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo

Kwenye kesi ambayo mashahidi thelathini na tano wataitwa kutoa ushahidi wao, upande wa mashtaka umeifahamisha mahakama kwamba marehemu Sharon alipigiwa simu na watu waliomdanganya kwamba wangemsaidia kumaliza shida zake za pesa.

Catherine Mwaniki kutoka afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma ameimbia mahakama kwamba wako na ushahidi wa kutosha kudhibitisha kwamba Gavana Obado pamoja na washtakiwa mwenza Michael Oyamo na Caspal Obiero walihusika katika kupanga na kutekeleza mauaji hayo.

Ripoti ya mpasuaji mkuu wa serikali Dr. Johansen Oduor imeonesha kwamba marehemu Sharon alikuwa na jeraha la kukatwa kwenye sikio lake la kushoto, jeraha la kudungwa kisu tumboni na kusabbaisha maini kutoka nje, majeraha kwenye sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo mgongoni, shingoni, mabegani na kupoteza damu nyingi.

Mfuko wa uzazi ulikuwa na mtoto ambaye tayari alikuwa amekufa huku upande mmoja ukiwa na jeraha.

Kesi hiyo itakayosikilizwa hadi Alhamisi Julai 15 inaanza baada ya Jaji Cecilia Githua kukataa kuridhia ombi la Obado aliyetaka kuhairsihwa kwake akihofia kuambukizwa corona.