Kiongozi wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi ameahidi kufufua uchumi wa taifa iwapo atachaguliwa kuwa rais kwenye uchaguzi mkuu wa 2022.

Mudavadi amesema maswala yanayahusiana na uchumi yanahitaji kuzamiwa kindani kupitia sera makhsusi.

Waziri wa huyo wa zamani wa fedha vile vile amewasuta wanasiasa anaosema wanazingatia maslahi yao ya binafsi badala ya kuinua uchumi unaowahusu Wakenya.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mudavadi ameonya dhidi ya kuingiza siasa katika maswala yanayohusiana na uchumi akisema  mwisho wake itakuwa majuto.