Mbunge wa Gilgil Martha Wangare amesema huenda serikali ilipoteza pesa nyingi katika ununuzi wa vitabu vya kusoma katika eneo hilo.

Mbunge huyo anasema nyingi ya shule zimepewa vitabu vya kusoma ambavyo hawakuhitaji na sasa vitabu hivyo havitumiki.

Wangare vile vile amelalamikia kucheweshwa kwa pesa za kufadhili masomo ya bure na kufanya vigumu kwa shule kuendelea na shughuli za kawaida.