Mahakama kuu imemuachilia huru mshukiwa sugu wa mauaji Philip Onyancha kutokana na kutokuwepo kwa ushahidi wa kutosha.

Onyancha alikuwa anakabiliwa na kesi juu ya mauaji ya wanawake wawili Catherine Chelangat na Jackline Chepngetich mwaka 2008.

Katika uamuzi wake, Jaji Jessie Lesiit amesema waendesha mashitaka katika kesi hiyo hawakutoa ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani mshukiwa.

Onyancha alikiri kuua wanawake 19 ikiwemo watoto lakini baadae mwaka 2014 akakana mashtaka matatu ya mauaji dhidi yake.