Tume ya huduma za walimu nchini (TSC) imeitisha awamu nyingine ya mazungumzo na walimu wiki ijayo kujadiliana kuhusu mkataba wa maelewano (CBA) baada ya mkutano wa kwanza kutibuka.

Afisa mkuu mtendaji wa TSC Nancy Macharia ameitisha mkutano wa pili na miungano ya walimu ya KNUT na KUPPET Jumanne ya Julai 13 kutafuta mwafaka.

Katika mkutano wa juma lililopita, TSC ilitoa mapendekezo yake lakini yakakataliwa na viongozi wa miungano hiyo akiwemo katibu mkuu wa KNUT Collins Oyuu kwa sababu walimu hawakupewa nyingeza ya mishahara.

Mkataba huo ni wa kati ya mwaka 2021-2025.