Kenya imetia saini mkataba wa Sh48b na shirika la fedha la Global Fund kusaidia katika kuafikia azimio la afya kwa wote katika miaka michache ijayo.

Katbu katika wizara ya afya Dkt. Rashid Aman anasema kupitia mkataba huo wa mwaka 2021-2024, Kenya itapata ufadhali utakaosaidia katika kupambana na magonjwa sugu kama vile Malaria, Ukimwi na kifua kikuu.

Mashirika ya Redcross na AMREF yamesema azimio kuu ni kupunguza maafa yanayosababaishwa na magonjwa hayo.