Polisi huko Nakuru wanamtafuta mwenzao Caroline Kangogo anayedaiwa kuhusika na mauaji ya constable John Ogweno wa kituo cha Polisi cha Nakuru.

Kangogo anadaiwa kuhepa baada ya mauaji hayo akiwa na bunduki ya marehemu aina ya Ceska iliyokuwa na risasi kumi na tano.

Mwili wa marehemu Ogweno ulipatikana ndani gari lake katika eneo la Kasarani ukiwa na majeraha ya risasi.

Naibu kamanda wa Polisi Nakuru Mashariki Phaton Analo amesema uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo umeanzishwa.

Maganda ya risasi inayoaminika kutumika kumuua afisa huyo yalipatikana kando ya mwili wake na inaaminika alipigwa risasi katika upande wa kulia wa kichwa na kufa kwa kuvuja damu nyingi.