Wizara ya fedha imetuma deni la Sh26.9b kwa serikali za kaunti pesa zilizokuwa zimesalia kwa kipindi cha matumizi ya fedha 2020/2021.

Waziri wa fedha Ukur Yatani amesema hii inafikisha Sh316.5b mgao wote ambao serikali za kaunti zimepokea.

Balozi Yatani ambaye awali alitoa Sh43.5b kwa kaunti amesema anawatarajia magavana kulipa madeni yote kwa wafanyibiashara kwa kutumia mfumo wa kidijitali wa IFMIS.

Magavana wamekuwa wakiteta kwamba kucheleweshwa kwa mgao huo umefanya vigumu kwa wao kuwajibikia majukumu yao ikiwemo ulipaji wa madeni na mishahara kwa wafanyikazi wake.