Rais Uhuru Kenyatta amefanya mazungumzo na mwenyeji wake wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Paris.

Mazungumzo hayo yameangazia kujenga uhusiano baina mataifa haya mawili sawa na kuisaidia Kenya kuwa na uwezo wa kujitengenezea chanjo.

Marais hao wawili vile vile wamejadiliana kuhusu hatua zilizopigwa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo upanuzi wa barabara ya kilomita 233 ya Rironi-Nakuru-Mau ulioanza Septemba mwaka jana.

Uhuru na Macron aidha wameangazia kongamano la kimataifa la elimu litakaloandaliwa mjini London kwa ushirikiano kati ya rais Kenyatta na waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson.