Mchakato wa kufanyia katiba marekebisho kupitia kwa mswada wa BBI haukuanzishwa na Rais Uhuru Kenyatta.

Ndio usemi wake Wakili Otiende Amollo ambaye ameliambia jopo la majaji saba wa mahakama ya rufaa kuwa mchakato huo ulianzishwa na mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed na mbunge wa zamani Dennis Waweru.

Kinyume na uamuzi wa mahakama kuu ulioharamisha mchakato wa BBI, Amollo amesema Rais Kenyatta aliunga mkono mchakato huo sawia na mkenya mwingine yeyote.

Amollo ambaye anawakilisha kiongozi wa ODM Raila Odinga kwenye kesi ya kupinga kuharamsihwa kwa mchakato wa BBI ameambia jopo hilo kuwa itakuwa ni vigumu kwa mwananchi wa kawaida pekee kufadhili marekebisho ya katiba kupitia kwa kura ya maamuzi.

Wakati uo huo,

Wakili wa rais Uhuru Kenyatta Waweru Gatonye amesema mahakama kuu ilimhukumu rais kuhusiana na mchakato huo pasipo kumpa nafasi ya kujitetea.