Jopo lililobuniwa kuwatafuta makamishna wapya wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini (IEBC) imewasaili watu 36 waliotuma maombi kujaza nafasi hizo.

Jopo hilo linaloongozwa na Dkt. Elizabeth Muli limewapa mtihani watu hao kubaini uwezo wao kuwajibikia majukumu yao kwa hekima na busara.

Mahojiano rasmi ya kuwasaka makamishna wanne wa IEBC yatafanyika kati ya Julai 7 na Julai 22 mwaka huu.