Kenya imerekodi maambukizi mapya 719 ya ugonjwa wa corona baada ya kupima sampuli 7,608 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Hii inafikisha 183,603 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini huku kiwango cha maambukizi kikiwa katika asilimia 9.5%.

Katika maambukizi hayo mapya, Nairobi imeandikisha visa 188, Busia 76, Kisii 57 na Siaya 53.

Wagonjwa 800 wamepona katika muda huo na kufikisha idadi hiyo 125,388 huku 9 zaidi wakifariki na kufikisha idadi hiyo kuwa 3,621.

Waliopata chanjo ya pili wamefikia 328,848 huku walipewa chanjo ya kwanza wakiwa 1,334,749.