Hatua zilizopigwa katika kuleta huduma karibu na mwananchi zimeangaziwa kwenye kongamano la Ugatuzi lililoandaliwa Jumanne jijini Nairobi.

Mwenyekiti wa baraza la magavana Martin Wambora amesema miongoni mwa hatua zilizopigwa ni katika sekta ya afya, kilimo na kuwasaidia walioathirika na janga la corona.

Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa vile vile alihutubia kongamano hilo ambapo alitoa wito kwa magavana kuwa wazi katika utendakazi wao.