Tume ya huduma za walimu nchini TSC imetangaza kuwa itawaajiri walimu 5,000 wa shule za upili na walimu 1,000 wa shule za msingi.

Tangazo hilo limetolewa na afisa mkuu mtendaji wa TSC Nancy Macharia katika hatua ambayo inalenga kupunguza uhaba wa walimu katika shule za umma unaoshuhudiwa kwa sasa.

Macharia amesema walimu hao pia watakuwa nguzo muhimu katika kufanikisha mpango wa serikali kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanaofanya mtihani wa darasa la nane wanajiunga na kidato cha kwanza.

Iwapo umehitimu na ungependa kujaza nafasi hizo unatakiwa kutuma maombi yako kupitia kwa wavuti wa tume hiyo tsc.go.ke kufikia tarehe 12 Julai mwaka huu.

Katika bajeti iliyosomwa hivi maajuzi, shughuli ya kuajiri walimu ilitengewa mgao washilingi million 2.5.