Mwanamume mmoja amehukumiwa jela miezi mitatu kwa kushindwa kurudisha Sh16,000 zilizotumwa kwa simu yake kimakosa.
Cyrus Nzoka Maithya alishtakiwa kwa makosa matatu ya wizi wa Sh16,463 alizopokea kutoka kwa Harriet Karimi mnamo Novemba 3, 2020.
Alikubali makosa yake mbele ya Hakimu Mkuu wa mahakama ya Nairobi Martha Nazushi na akapewa nafasi ya kurejesha pesa hizo ila akashindwa.
Akijitetea, jamaa huyo aliambia mahakama kwamba yeye ni baba wa watoto wawili wanaomtegemea na akaomba asamehewe.
Hakimu huyo alimpa kifungo cha miezi mitatu jela au alipe faini ya Sh20,000.