Mjumbe wa miundo mbinu na maendeleo katika muungano wa Afrika (AU) Raila Odinga yuko nchini Ethopia kwa mkutano kuhusu ujenzi wa bandari ya Lamu itakayounganisha Sudan Kusini na Ethopia.

Odinga amesema ujenzi wa bandari hiyo utakuwa mwanzo mpya kwa uchukuzi anaosema utapiga jeki maendeleo ya kanda hii.

Mkutano huo unajiri baada ya rais Uhuru Kenyatta kuzindua sehemu ya kwanza ya ujenzi wa bandari hiyo majuma machache yaliyopita.

Waziri huyo mkuu wa zamani na kinara wa chama cha ODM amewarai viongozi wengine barani kuunga mkono ujenzi wa bandari hiyo.