Kenya imeripoti maambukizi mapya 287 ya ugonjwa wa corona kati ya sampuli 2,699 zilizopimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Kiwango cha maambukizi nchini kwa sasa kiko katika asilimia 10.6% huku idadi ya visa vya ugonjwa huo ikifikia 182,884.

Wagonjwa 152 wamepona na kufikisha idadi hiyo kuwa 124, 588 huku 17 zaidi wakifariki na kufikisha idadi hiyo kuwa 3,612.

Idadi ya wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali ni 1,062 huku 6,730 wakiwa chini ya mpango wa kushughulikiwa nyumbani.