Licha ya pingamizi kutoka kwa wadau mbalimbali, katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini (COTU) Francis Atwoli amesema atazidi kushinikiza kuhairishwa kwa uchaguzi mkuu ujao iwapo mchakato wa BBI utasimamishwa na mahakama.

Akizungumza alipofungua rasmi kongamano la wanahabari kutoka Afrika Mashariki jijini Nairobi, Atwoli amesema BBI ni muhimu kwa taifa hili kabla ya uchaguzi.

Atwoli vile vile ametoa wito kwa vijana kukumbatia ubunifu kama njia mojawapo ya kujipa ajira.

Mahahama Jumanne hii inatazamiwa kuanza kusikilzia rufaa iliyowasilishwa kupinga uamuzi wa mahakama kuu uliosimamisha mchakato huo wa kurekebisha katiba.