Hali ya huzuni imetanda wakati wa ibada ya wafu kwa aliyekuwa mbunge wa Gem Jakoyo Midiwo.

Ibada hiyo imeandaliwa katika kanisa la Christ Is The Answer Ministry na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo binamuye Raila Odinga, Musalia Mudavadi na Kalonzo Musyoka ambao kwa huzuni wamemtaja marehemu kama rafiki.

Lakini nini kilimuua Jakoyo Midiwo?

Nduguye Profesa George Midiwo amefichua kwamba mwanasiasa huyo alifariki baada ya figo zake kukataa kufanya kazi hali iliyotatiza sehemu zingine za mwili.

Midiwo atazikwa Jumamosi hii ya Juni 26 nyumbani kwake Akala, kaunti ya Siaya.

Jakoyo Midiwo alifariki Juni 14 akiwa Nairobi Hospital alipokimbizwa kwa matibabu ya dharura.