Familia moja katika kijiji cha Katunoi eneo bunge la Baringo ya Kati inaomboleza kifo cha wapendewa wao wawili waliofariki baada ya kufumwa mshale wenye sumu.

Alphonce Kipchumba na mkewe Melvin Rotich walifumwa mshale na mshukiwa Alexender Kipchumba baada ya kuzozania kipande chake cha ardhi.

Inaarifkiwa kwamba mshukiwa ambaye kwa sasa anazuiliwa na maafisa wa Polisi mjini Kabarnet alitaka kuuza shamba hilo baada yake kugundua kwamba alikua ameambukizwa virusi vya Ukimwi.

Kisa hicho kimethibitishwa na OCPD Baringo ya Kati Francis Gachoki ambaye amesema kuwa mshukiwa alikamatwa eneo la Kaptimbor viungani mwa mji wa Kabarnet akiwa na uta pamoja na mishale minne yenye sumu.

Miili ya wawili hao inahifadhiwa katika chumba Cha wafu kwenye hospitali ya Rufaa ya Baringo.