Mahakama imekubali vikao vya kusikilizwa kwa kesi dhidi ya aliyekuwa waziri wa Michezo Rashid Echesa kusikilizwa faraghani.

Mahakama ya Nairobi imeridhia ombi la upande wa mashtaka uliotaka mashahidi wawili kutoka wizara ya Ulinzi kutoa ushahidi wao kisiri.

Kwenye kesi hiyo, Echesa pamoja na wenzake wanne wameshtakiwa kwenye sakata inayohusiana na zabuni feki ya silaha.

Mwanasiasa huyo na washtakiwa wenza waliachiliwa kwa dhamana baada ya kukanusha mashtaka 12 kwenye sakata hiyo inayogharimu Sh39.5b.