Kenya imeripoti maambukizi mapya 583 ya corona baada ya kupima sampuli 6,686 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Kiwango cha maambukizi kiko katika asilimia 8.7% huku visa vya ugonjwa huo nchini vikongezeka na kufikia 179,876.

Nairobi imerekodi maambukizi mapya 111, Siaya 57, Kisumu 51, Kericho 46, Mombasa 43, Busia 39, Nakuru 25, Nyamira 24, Kakamega 21, Homa Bay 20, Vihiga 19, Trans Nzoia 17, Laikipia 12, Kilifi & Bungoma 11, Makueni 10, Nandi 9, Kajiado & Kiambu 7, Bomet, Machakos & Taita Taveta 5, Kisii 4.

Wagonjwa 85 zaidi wamepona na kufikisha idadi hiyo kuwa 123,050 huku 23 zaidi wakifariki na kufikisha idadi hiyo kuwa 3,484.

Idadi ya wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali ni 1,098 huku wengine 5,669 wakishughulikiwa nyumbani.